Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya usimamizi wa utangazaji wa mashirika ya serikali ya Marekani – BBG – ambayo inasimamia shirika la habari la Sauti ya Amerika (VOA), John Lansing, ametoa wito kwa rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, kubatilisha uamuzi wa serikali yake, wa kupiga marufuku matangazo ya VOA nchini humo, kama njia ya kuimarisha usalama, kuzuia ghasia na kulinda raia wa Burundi.
Lansing amesema kuwa bodi hiyo itaendelea kuwaunga mkono raia wa Burundi kwa kutoa matangazo ya kuaminika na yasiyopotosha.
Hayo yamejiri baada ya serikali ya Burundi ya kusitisha matangazo ya Idhaa ya Sauti Amerika kwa muda wa miezi sita nchini humo kuanzia jana Jumatatu.
“Ingawa VOA pia hutangaza katika mawimbi ya masafa mafupi, televisheni na kupitia mtandao katika nchi hiyo, hapana shaka kwamba matangazo ya redio kupitia masafa ya FM ndiyo maarufu zaidi nchini Burundi,”amesema Lansing
Hata hivyo, ameongeza kuwa raia wa Burundi wamekuwa wakitegemea Sauti ya Amerika kwa matangazo yasiyoegemea upande wowote, wakati nchi hiyo ikikabiliwa na mzozo unaoendelea wa kisiasa.
-
Odinga awapa neno wafuasi wake
-
Wizara ya Afya yatoa Kondomu 3,000
-
Rais asema Taifa lakumbwa na msiba mkubwa