Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amewasihi wafuasi wake wasitishe kampeni ya kususia bidhaa na biashara za kampuni zilizohusishwa kuwa na uhusiano na chama tawala cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta.

Odinga ametoa tamko hilo katika sikukuu ya Mei Mosi zilizofanyika katika mji mkuu wa Kenya jijini Nairobi.

“Tulikuwa na hasira nyingi kwa yale makampuni yaliyokuwa yanaunga mkono serikali ya Jubilee. tulisema ni makampuni ambayo yanatesa watu wetu, ambayo yamekataa kukubali uamuzi wa wananchi na tukasema watu wetu wote wasusie bidhaa za kampuni hizo. Sasa tumeshikana mkono na Uhuru, tumekubaliana kufanya kazi pamoja tusuruhishe mambo, na tumeweka sasa kamati ya ushauri ya kuleta suluhu ya kudumu,”amesema Odinga

Hata hivyo, tangazo la kususia bidhaa za wanaotajwa kuwa washirika wa chama tawala lilitolewa Novemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu ambao ulibatilishwa na Mahakama ya juu nchini humo kwa madai kuwa ulikuwa na dosari.

 

 

 

Waumini 16 wauawa na watu wenye silaha waliovamia kanisa
Ndege ya jeshi la Urusi yazua taharuki nyuma ya ndege ya Marekani