Bweni la shule ya Sekondari ya wasichana ya Uchira Islamic iliyoko wilaya ya Moshi vijijini mkoa wa kilimanjaro limeteketea kwa moto jioni ya Octoba 16, 2020 huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana, hakuna kofo wala madhara kwa mawanafunzi yoyote.
Ispekta Abrahamu Ntezidyo kutoka jeshi la zimamoto mkoa wa kilimanjaro amesema kuwa taarifa moto waliziata jana jioni majira ya saa 12:00, ambapo amesema moto umetekeza jumla ya vitanda 25 amabvyo walikuwa wakilalia wanafunzi 50.
” Athari kubwa ni kwenye vitu vya wanafunzi na vitanda, wanafunzi hawakuwepo bwenini walikuwa wameenda msikiti kwaajili ya swala ya jioni, mpaka sasa tunaendelea na uchunguzi wa moto huo ili kubaini chanzo cha moto ulipoanzia” amesema Ispekta Ntezidyo.
‘Hapa wanafunzi wapo katika hali ya mstuko mkakati uliopo tunakagua shule moja baada ya nyingine kwa kushirikiana na vyombo vingine na hata hii iliyoungua tunavyozungumza imekaguliwa juzi tuu haata wiki haijaisha, lakini bahati mbaya imeungua vyanzo vya moto viko vingi kuna umeme, hujuma kuna vingine vinasababishwa kwa makusudi”amesema Ispekta Ntezidyo.