Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere imesema kuwa mapungufu ya udhibiti kwenye Mfuko wa madai ya Bima ya Afya yanaonesha madai ya wanaume 56 walipata huduma ya upasuaji au za kawaida za kujifungua wakati huduma hizo zinatolewa kwa wanawake.
Pia wanachama 444 walipata huduma ya kuchunguzwa picha kamili ya damu ( full blood picture), zaidi ya mara moja kwa siku hadi mara 30 kwenye kituo kimoja.
Akizungumza jijini Dodoma na waandishi wa habari wakati akiwasilisha ripoti yake ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2020 /2021 CAG Kichere amesema kuwa kuwapo kwa malipo ya madai yaliyorudiwa pamoja na madai yanayoonesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), walipokea miwani ya kusomea zaidi ya mara moja wakati utaratibu unaruhusu kutoa miwani mara moja kwa mwaka.
Kichere ameongeza kuwa udhaifu huo umesababishwa na kukosekana kwa udhibiti katika mfumo wa madai iliyosababisha hasara ya shilingi milioni 14.41 katika mfuko.
” Ninapendekeza Mfuko wa Bima ya Afya kurejesha kiasi kilichopotea kutoka kwa watoa huduma za afya husika,kuboresha mfuko wa madai wa CMIS ili kuhakikisha unasaidia maafisa wanaohusika kuangalia uhalali wa madai yaliyowasilishwa.