Kiungo kati kutoka nchini Ecuador na klabu ya  wa Brighton, Moisés Isaac Caicedo Corozo na klabu ya Brighton & Hove Albion, amekiri kuwa hataweza kukataa kuhamia Chelsea msimu huu wa joto.

Caicedo ndiye anayelengwa zaidi na The Blues ili kujaza safu yake ya kiungo baada ya kuondoka kwa Mason Mount, Mateo Kovacic, N’Golo Kante na Ruben Loftus-Cheek, na kwa muda mrefu wamekuwa kwenye mazungumzo na Brighton kuhusu kumsajili msimu huu wa joto.

Kinachobaki ni bei ya Brighton ya Pauni Milioni 100 ambayo ni ya chini kuliko ile ya uhamisho wa Declan Rice kwenda Arsenal.

Kiungo huyo wa kati wa West Ham amegharimu ada ya pauni milioni 105 na Brighton hawaamini kwamba, Caicedo anatakiwa kuwa nafuu zaidi.

Mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yameonekana kuwa magumu, lakini Chelsea ilionekana kutokumbana na matatizo kama hayo katika mazungumzo na Caicedo, ambaye alikubali kuwa hataweza kuwakataa The Blues msimu huu wa joto.

“Ni timu kubwa….., hiyo ni kweli,” alisema Caicedo akimwambia mwandishi, Maria Jose Flores alipoulizwa kuhusu nia ya Chelsea.

“Timu ya kihistoria na siwezi kusema hapana, kwa sababu ni timu kubwa, ya kihistoria na nzuri.

“Mji pia ni mzuri. Una kila kitu kizuri.”

Brighton wameonyesha nia ya kuona Chelsea wakitoa ofa kwa beki wa kati Levi Colwill kama sehemu ya biashara hiyo ya kumnunua Caicedo, lakini The Blues wameweka wazi kuwa hawakubaliani na wazo kama hilo.

Colwill aling’ara msimu uliopita akiwa kwa mkopo Brighton na wanataka kumbakiza, huku Liverpool zikimwania pia.

Colwill anatarajiwa kuripoti kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya akiwa na Chelsea katika siku zijazo na atazungumza na kocha, Mauricio Pochettino kuhusu hatma yake katika klabu hiyo, baada ya kuzungumza waziwazi wakati wa majira ya joto kuhusu nia yake ya kuona anacheza kikosi cha kwanza na wanataka kumna Manchester City

“Lazima nicheze mwisho wa siku,” aliwaambia wanahabari baada ya msimu wake wa ushindi wa Ulaya akiwa na timu ya taifa ya Vijana ya England chini ya umri wa miaka 21.

Chelsea ina wachezaji kadhaa wa kati kwenye rada zao msimu huu wa joto lakini kwa sasa wanaelekeza nguvu zao kwa Caicedo.

Lionel Messi kutambulishwa Inter Miami CF
Wadau malezi ya Watoto ishirikisheni TAMISEMI - Mpanju