Klabu ya Manchester United imethibitisha kuwa kiungo wake, Casemiro amerejea mazoezini baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Kiungo huyo amekosa mechi nane hadi sasa kutokana na jeraha la misuli ya paja alilopata wakati wa kichapo cha mabao 3-0 kutoka Newcastle United kwenye Kombe la Carabao Novemba Mosi, mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye tovuti rasmi ya klabu, Man Utd ilitangaza kwamba hatimaye Casemiro amerejea mazoezini: “Casemiro ameanza mazoezi ya uwanjani, huku Mbrazil huyo akiongeza ahueni kwa Manchester United.”

Siku ya Jumapili, kiungo huyo alionekana akifanya mazoezi peke yake kwenye Uwanja wa Carrington.

Jeraha hilo la msuli wa paja lilikuwa la pili kuugua kwa mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid huku pia akiumia kifundo cha mguu alipokuwa akiichezea Brazil dhidi ya Venezuela.

Akiwa amekosa mechi tatu za klabu kutokana na jeraha la kifundo cha mguu, kiungo huyo alirejea uwanjani dhidi ya Newcastle, lakini akaambulia patupu tena wakati wa mapumziko kwenye mechi iliyopigwa Old Trafford.

Kurejea kwa Casemiro mazoezini, ingawa bado hajakichezea kikosi cha kwanza, ni habari njema kwa Mashetani Wekundu na kunaweza kumaaniisha kwamba Mbrazil huyo anaweza kurejea dimbani mapema kuliko ilivyotarajiwa.

Akizungumza mapema Mwezi Novemba kuhusu ni lini alitarajia Casemiro na Lisandro Martinez kurejea dimbani, Kocha Erik ten Hag alisema kwamba hakuwategemea wawili hao kurejea uwanjani kabla ya Krismasi.

Aweso Mgeni rasmi Mkutano Wadau Sekta ya Maji
Young Africans, Simba SC zarejea Ligi Kuu