Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema sera ya afya na Elimu bure Zanzibar itaendelea kutekelezwa kupitia ilani ya uchaguzi ya Mwaka 2020-2025.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi – CCM ngazi ya Shina, Wajumbe wa Halmashauri Jimbo, Wilaya na Mkoa.

Amesema, Chama Cha Mapinduzi ndicho chama kinachofaa kuongoza Zanzibar huku akiwahimiza wananchi kuwa na umoja na mshikamano na kujiandaa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kuchagua Viongozi wenye kuwaletea maendeleo.

Rais Dk. Mwinyi alihitimisha ziara hiyo kwa kutembelea na kukagua miradi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwemo eneo la Kituo cha Mafuta Mahonda, kitega uchumi cha CCM Nungwi, eneo la CCM Afisi kuu Kiwengwa, Shamba la CCM Afisi kuu Kilombero.

Picha: Wananchi walivyompa pole Museveni geti la Ikulu
Ayanfe kuitikisa Afrika Mashariki