Chama cha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani cha CDU kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwisho wa mikoa katika jimbo la Saxony-Anhalt kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kwanza katika miaka 16 bila kumhusisha kansela huyo mkongwe
Matokeo ya mwanzo yanaonyesha kuwa chama cha CDU chini ya kiongozi mpya Armin Laschet kimeshinda karibu asilimia 37 ya uchaguzi wa jimbo la Saxony-Anhalt, dhidi ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia AfD katika nafasi ya pili.
Ushindi wa CDU chini ya waziri mkuu wa Saxony-Anhalt Reiner Haseloff unaonyesha ongezeko la asilimia 7 tangu uchaguzi wa mwisho 2016.
“Watu wa Saxony-Anhalt wametuma ujumbe wa wazi leo, mkoa wa Saxony-Anhalt unabaki imara katika kitovu cha siasa, wapiga kura wameamua kuwa Reiner Haseloff ataendelea kuwa Gavana wa Jimbo na kuliongoza jimbo hili zuri kwa siku zijazo, CDU ina wajibu wa wazi wa kuongoza sisi ndio chama chenye nguvu kubwa kisiasa na matokeo yetu leo ni mazuri sana.” Amesema katibu mkuu wa CDU Paul Ziemiak
Chama cha Merkel CDU kwa miaka mingi kimekua nguvu kubwa katika jimbo la Saxony-Anhalt la iliyokuwa Ujerumani Mashariki, kwa kushinda uchaguzi wote wa eneo hilo isipokuwa mmoja tu tangu kuungana kwa Ujerumani mbili mwaka wa 1990.
Laschet amabye aliteuliwa kuwa mgombea wa kihifaidhina wa wadhina wa ukansela mwezi april, alirithi mfululizo wa matatizo ikiwemo hasira kuhusiana na namna serikali ililishughulikia janga la corona na kashfa ya rushwa inayohusisha kandarasi za mashaka za barakoa za kuzuia virusi vya corona