Michuano ya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa Wanawake ukanda wa Afrika Mashariki na kati CECAFA, imesogezwa mbele.

CECAFA wamesogeza mbele tarehe ya kuanza kwa Michuano hiyo itakayofanyika Mjini Nairobi nchini Kenya, huku ikishindwa kujata tarehe mpya.

Awali Michuano hiyo ilipangwa kuanza Julai 17 na kufikia tamati Agosti Mosi.

Katika michuano hiyo Tanzania itawakilishwana Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2020-21 Simba Queens, ambao wamepangwa ‘KUNDI A’ pamoja na PVP FC ya Burundi na Mabingwa wa Uganda Lady Doves WFC.

Simba Queens inaendelea na maandalizi kuelekea michuano hiyo ya CACAFA, na jana Jumanne (Julai 13) ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars).

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, ulishuhudia Simba Queens ikifungwa mabao 2-1.

Mugalu: Nataka kuwa mfungaji bora Tanzania
KMC FC kushuka dimba la Uhuru kuikabili JKT Tanzania