Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa mawakala wake wananyanyaswa lakini kinasubiri matokeo yatangazwe ili kiweze kuchukua hatua.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Bara, John Mnyika ambapo ameitupia lawama Tume ya Uchaguzi.

Amesema kuwa wasimamizi wengi wa uchaguzi ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao tayari wameshapewa maelekezo ya kufanya kila kituo.

“Niwaambie waandishi wa habari kuna maafisa wameletwa kwa ajili ya kuandaa mchakato mzima wa kuchakachua kura,” amesema Mnyika

Hata hivyo, Mnyika amesema kuwa sehemu kubwa ya wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)


Video: Hivi ndivyo Jeshi la Polisi lilivyojipanga kuelekea Uchaguzi leo, IGP Sirro afunguka

Video: Mgombea ajiuzulu dakika chache kabla ya uchaguzi
Chadema walia kuhujumiwa na CCM Ukonga