Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole anapaswa ahojiwe kuhusu kauli yake aliyoitoa kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyepigwa risasi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Itikadi na Mawasiliano wa Mambo ya Nje, John Mrema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kiongozi huyo anatakiwa ahojiwe kwakuwa inawezekana anajua mengi kuhusu kifo cha binti huyo.

Amesema kuwa matukio ya kutekwa na kuuawa umekuwa ni utamaduni mpya katika siasa za Tanzania kwani hapo awali nhaikuwepo.

“Tumesikitishwa sana na tamko la ajabu la Humphrey Polepole, ni tamko la ajabu kweli kweli la kusema Chadema tulikodi vijana kwenye magari kwa ajili ya maandamano, kitu hiki sio cha kweli hata kdogo,”amesema Mrema

Hata hivyo, Mrema amelitaka jeshi la polisi kumhoji Polepole kwani inawezekana akawa anajua kile kilichotokea kwa mwanafunzi huyo aliyepigwa risasi.

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 19, 2018
Serikali yajitosa kugharamia mazishi ya Akwilina