Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC Clatous Chama ‘Mwmba wa Lusaka’ ameanza kutoa maelekezo magumu kwa vitendo kwa wachezaji wenzake ndani ya Uwanja katika mechi za ushindani.

Raia huyo wa Zambia anashikilia rekodi ya kuwa namba moja katika kutengeneza pasi za mwisho msimu wa 2022/23 alipotoa pasi 14 na kufunga mabao manne.

Msimu mpya wa 2023/24 tayari kaanza makeke yake ilikuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa alipofungua akaunti yake ya mabao kwa kufunga bao moja akitumia maelekezo ya pasi ngumu kutoka kwa mshikaji wake Luis Miquissone ilikuwa dakika ya 80 kwa mguu wa kushoto.

Hakuwa mnyonge katika mchezo wa ligi Agosti 20 dhidi ya Dodoma Jiji Uwanja wa Uhuru alitoa maelekezo magumu kwa kutoa pasi ya upendo kwa nahodha msaidizi Mohamed Hussein Zímbwe Jr dakika ya 43 iliyotumwa kwa Jean Baleke aliyefunga bao katika mchezo huo.

Mbali na pasi hiyo iliyokuwa chanzo cha mashabiki wa Simba SC kunyanyuka kwenye viti alitoa maelekezo mengine dakika ya 69 kwa mshikaji wake Luis ambaye alikosa kufunga nafasi hiyo na alifanya majaribio dakika ya 23, 79 zote hazikuleta matunda kwenye mchezo huo.

Serikali kuendeleza udumishaji wa Demokrasia Nchini
Ubunifu kusaidia vyuo vya Maendeleo kukusanya mapato