Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama ‘Triple C’ amesema hakuna namna kwa wachezaji wanaounda kikosi cha Simba SC, zaidi ya kupambana bila kuchoka msimu huu 2022/23.

Kikosi cha Simba SC kina Deni kubwa kwa Mashabiki na Wanachama, baada ya kupoteza Mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ msimu uliopita, tena mikononi mwa watani zao wa jadi Young Africas.

Chama amesema timu yao inapaswa kufanya vizuri msimu huu ili kurejesha hadhi na thamani ndani na nje ya Uwanja, na mpango huo unatakiwa kuonekana kwa vitendo na sio maneno pekee yake.

Amesema anaamini kikosi chao kina uwezo wa kufanya lolote ndani ya Uwanja ili kupata ushindi ambao utawarudisha furaha Mashabiki na Wanachama wao, na ndio maana viongozi wao waliingia sokoni na kusajili wachezaji wenye viwango bora.

“Msimu huu Simba SC inahitaji kufanya vizuri na kushinda mataji yote, hayo hayatawezekana bila ya wachezaji kuwa katika viwango bora ili kupigania malengo yetu, kwani si kazi rahisi kutokana na ushindani uliopo,”

“Nilichoonesha katika Michezo ya nyuma kimeshapita, nimejipanga kufanya vingine bora ili timu iweze kushinda kila mchezo uliokuwa mbele yetu, na yote hayo yatawezekana kutokana na ushirikiano wa wachezaji wenzangu.”

“Ukiangalia ubora wa wachezaji tuliokuwepo msimu uliopita na wale wapya waliosajiliwa msimu huu, kuna kitu kitaongezeka katika ushindani na kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita katika michuano yote.”

mesema Chama aliyerejea Simba SC wakati wa Dirisha Dogo la usajili mapema mwaka huu akitokea RS Berkane alikouzwa mwanzoni mwa msimu uliopita.

Simba SC itarejea tena katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara Jumatano (Septemba 07), kucheza dhidi ya KMC FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Tayari Simba SC imeshajikusanyia alama sita, kufuatia kushinda michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold FC iliyokubali kichapo 3-0, kisha ikailiza Kagera Sugar 2-0.

Kisinda afunguka kilichomrusha Young Africans
Clatous Chama ampagawisha Zoran Maki