Hatimaye Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Tuisila Kisinda ‘TK Master’ amefunguka sababu zilizomng’oa RS Berkane na kukubali kurudi Young Africans.

Kisinda alithibishwa kurudi Young Africans usiku wa kuamkia jana Alhamis (Septemba Mosi), sekunde chache kabla ya Dirisha la Usajili Tanzania Bara kufungwa rasmi.

Kiungo huyo amesema alikua katika mazingira magumu ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha RS Berkane, na ilifikia wakati aliomba nafasi ya kuondoka klabuni hapo ijitokeze, hivyo kusajiliwa kwake Young Africans kumemfariji sana.

“Haikuwa ngumu kukubali kurudi Young Africans, kwa sababu ndio klabu iliyonipa jina na kujulikana hadi Morocco, ninamini kurudi kwangu kutainufaisha sana klabu hii, ambayo ninaipdenda na kuithamini sana.”

“Nilikua katika hali ngumu nchini Morocco, ilifikia hatua nilikuwa naomba nafasi ya kurudi Young Africans itokee, kweli imetokea na imenifariji kutokana na kutambua wazi kuwa nimerudi nyumbani ninakokupenda.”

“Ninaungana tena na familia yangu ya Young Africans, ninaahidi nitapambana kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu ili kuendelea kuipa heshima klabu hii.”

“Young Africans hii ni tofauti sana na ile niliyoiacha, ina kila kitu ndani na nje ya Uwanjani, hivyo nina uhakika nitaongeza kitu katika mapambano ya kuendelea kulinda heshima ya klabu hii ambayo kwa sasa ndio Mfalme wa Soka la Tanzania.” amesema Kisinda ambaye msimu uliopita akiwa sehemu ya kikosi cha RS Berkane kilichotwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika

Kisinda anatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam wakati wowote kabla ya kuendelea na Ligi Kuu Tanzania Bara mwanzoni mwa juma lijalo, akitokea nchini Morocco.

Usajili wa Kisinda katika kikosi cha Wananachi kumelifanya Benchi la Ufundi kukuna vichwa juu ya nyota gani aachwe ili kukidhi matakwa ya kikanuni.

Hata hivyo inaelezwa kuwa jina la Mshambuliji kutoka nchini Zambia Lazarius Kambole limekatwa kupisha usajili wa ‘TK Master’, huku Jesus Moloko na Heritier Makambo wakiponea chupuchupu.

TAWA yawasilisha taarifa za uhifadhi kwa Serikali
Chama: Tutapambana ili kupata tunachokitaka