Shirika la Afya Duniani WHO limependekeza chanjo ya malaria ianze kutumika kwa watoto barani Afrika.
Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema Chanjo hiyo ni hatua muhimu kwa Sayansi, afya ya watoto na udhibiti wa Malaria ikiwa lengo kuu ni kuokoa maelfu ya maisha kila mwaka.
WHO imesema chanjo ya RTS,S inapaswa kutolewa kote kusini mwa jangwa la Sahara na Kanda nyingine zenye maambukizi ya wastani hadi ya juu na hii ni baada ya mafanikio katika majaribio yaliyofanyika Ghana, Kenya, na Malawi.
Hatua hii imetajwa kuwa ya kihistoria katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa malaria ambao umeua watoto zaidi ya 260000 barani humo kwa mwaka 2019.
Chanjo hiyo ilitengezewa katika Chuo Kikuu cha Oxford kilichoko Uingereza na Taasisi ya Chanjo iliyoko India na hii ni awamu ya tatu ambayo nchi ya Tanzania inatarajiwa kuwa miongoni mwa nchi shiriki.