Shirika la kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori  WWF limetoa elimu na vifaa aina ya vilipuzi 400  vya kukabiliana na tembo waharibifu katika vijiji vitano vilivyopo Halmashauri ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati anamkabidhi vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mhifadhi na Melimishaji wa WWF Ally Thabiti Mbugi  amesema wametoa elimu ya kujikinga na wanyama waharibifu hususani tembo kwa wananchi ili kukabiliana na uharibifu bila kuleta madhara kwa wanyama.

Aidha vifaa vingine vilivyokabidhiwa ni pamoja na magunia ya pilipili,vilipuzi kamba na vitambaa vya pamba ambavyo vinatumika katika utengenezaji wa wigo wa pilipili ambao unasaidia kuzuia tembo wasiharibu mashamba ya wananchi.

‘’Hivi sasa tunakaribia msimu wa kilimo hivyo tumetoa elimu na vifaa mapema kabla ya uharibifu kufanyika,hata hivyo katika Mkoa wa Ruvuma tutatoa vilipuzi 800 katika wilaya za Namtumbo na Tunduru ambapo kuna uharibifu wa mazao unaofanywa na tembo,pia tumetoa mbegu za pilipili ili wananchi mwakani wasipate tabu,” Amesema Mhifadhi Thabiti.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt.Julius Ningu amewapongeza na kuwashukuru WWF kwa msaada huo kutokana na ukweli kuwa Namtumbo imeathirika na wanyamapori waharibifu wa mazao.

Hali tete FC Barcelona, Coutinho kurudi England
Chanjo ya Malaria kutolewa kwa watoto