Kiungo kutoka nchini Brazil na klabu ya Barcelona, Philippe Coutinho huenda akaihama klabu hiyo na kurejea nchini England wakati wa majira ya baridi (Dirisha Dogo) mwezi Januari mwaka 2022.

Kiungo huyo anatajwa kuwaniwa na klabu za jijini London, Arsenal na Tottenham Hotspur, na inadaiwa tayari mazungumzo ya awali ya uhamisho wake yameanza.

Coutinho amekuwa na mazingira magumu ya kucheza tangu kuanza kwa msimu huu 2021/22, kwani hadi sasa amecheza dakika 82 pekee za michuano yote ikiwa ni baada ya kurejea kutoka kwenye majeraha yaliyokuwa yanamsumbua tangu msimu uliopita.

Amekuwa hapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza tangu atue kwenye viunga hivyo vya Camp Nou mwaka 2018 kwa dau la pauni milioni 145 lililovunja rekodi ya mauzo kwa upande wa Ligi Kuu England.

Taarifa zinadai mchezaji huyo angependa zaidi kurejea Liverpool, lakini wababe hao hawajaonyesha mpango wa kumchukua kiungo huyo wa ushambuliaji aliyewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu mfululizo kuanzia mwaka 2014 hadi 2016.

Kiungo huyo aliwahi kushinda taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 2020 akiwa na Bayern Munich aliyokuwa anaitumikia kwa mkopo na kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Barca alifunga mabao mawili.

Simba SC yaanika mipango ya kuisasambua Jwaneng Galaxy
Tembo waharibifu wapatiwa suluhu