Hayimaye Uongozi wa Azam FC umevunja ukimya kuhusu suala la kuwasimamisha wachezaji watatu waandamizi wa klabu hiyo, baada ya taarifa hizo kuripotiwa kama tetesi.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano (Oktoba 06) usiku na kuthibitishwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria, imewataja wachezaji hao kuwa ni Agrey Morris, Mudathir Yahya na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Watatu hao wanadaiwa kuonesha utovu wa nidhamu kwa meneja wa timu kabla na baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Horseed FC ya Somalia.

Biteko awataka wafanyabiashara wa madini kusajili mikataba
Kennedy Juma asivyokauka midomoni mwa wadau