Mabingwa wa Soka wa Tanzania Bara Simba SC, wamejinasibu kuwa tayari kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya kwanza dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Simba SC wataanzia ugenini mjini Gaberone Oktoba 15, kisha watamalizia nyumbani jijini Dar es salaam Oktoba 22, mwaka huu, kwa kucheza mchezo wa mkondo wa pili Uwanja wa Benjamin mkapa.

Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, amesema Uongozi unaendelea kufanya maandalizi kuelekea mchezo huo, na benchi la ufundi chini ya Kocha Didier Gomez linakamilisha mpango wa kuwaandaa wachezaji kabla ya safari ya kuelekea Botswana.

“Kama uongozi tunaendelea kufanya maandalizi ya kikosi chetu kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, ni jambo zuri kuwa tunauelekea mchezo huu tukiwa na ari ya ushindi baada ya kuifunga Dodoma Jiji kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara.

“Bahati nzuri kwetu ni kwamba wachezaji wetu wana uzoefu na mashindano haya, lakini ubora wa kikosi tulichonacho ni sababu tosha ya kufanya vizuri.” amesema Mangungu

Msimu uliopita, Simba SC iliishia Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika , huku ikiwa ni mara ya pili baada ya kufanya hivyo msimu wa 2018/19.

Asante Kotoko kuipima Young Africans
Hali tete FC Barcelona, Coutinho kurudi England