Naibu Waziri wa Maji,] Mhandisi Maryprisca Mahundi] amemuagiza Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Masasi kuhakikisha Vijiji nane vya Mnavira, Manyuri, Mkaliwata Chipingo, chikolopola, Mapili, Namyomyo na Raha Leo vinapata huduma ya maji kadri ya usanifu wake.

Mhandisi Mahundi ameyasema hayo Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ambayo alitembelea na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.9.

Kadhalika Mhandisi Mahundi ameagiza vijiji hivyo viweze kufikiwa na huduma ya maji kabla ya mwezi Februari, 2024.

Naye Mbunge wa Jimbo la Lulindi, Issa Mchungaela ameishukru Serikali kwa kutekeleza mradi huo, kupitia chanzo cha maji cha Mto Ruvuma

Hata hivyo, Mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata ni miongoni mwa miradi ambayo inatumia chanzo cha maji cha Mto Ruvuma.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 18, 2023
Miezi 10 tangu afariki: Hatimaye Lokassa ya Mbongou azikwa