Saa chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa, klabu ya Chelsea ya jijini London imeripotiwa kuwa katika mpango wa kurejesha aliyewahi kuwa beki wao kutoka nchini Brazil David Luiz kwa ada ya Pauni Milioni 32.

Mbrazil huyo aliondoka Chelsea Juni 2014 na kujiunga na mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) kwa dau lililovunja rekodi ya Dunia upande wa mabeki mabeki ambalo lilikuwa Pauni Milioni 50.

Chelsea inahaha kutafuta beki wa kati hasa baada ya kukataliwa kuwasajili Alessio Romagnoli wa AC Milan na mlinzi wa Napoli, Kalidou Koulibaly.

Yametimia, Joe Hart Amalizana Na Torino FC
Wayne Rooney Kustaafu Soka Mwaka 2018