Klabu ya Chelsea ina mpango wa kuwasilisha ofa mpya Brighton ya zaidi Pauni 70 milioni ili kuipata huduma ya kiungo wa timu hiyo, Moises Caicedo dirisha hili.

Taarifa zinadai tayari Chelsea imeshafanya makubaliano binafsi na Caicedo na kinachokwamisha dili hilo ni makubaliano baina ya timu mbili na tangu juma lililopita mmoja wa wakurugenzi wa michezo wa matajiri hao amekuwa kwenye mazungumzo ya kina na Brighton.

Awali Chelsea iliwasilisha ofa ya Pauni 60 milioni iliyokataliwa na taarifa zinadai mabosi wa Brighton wameshikilia msimamo wa kutaka zaidi ya Pauni 100 milioni ili kumuuza nyota huyu.

Msimamo wa kutaka Pauni 100 milioni na zaidi unachagizwa zaidi na kitendo cha Arsenal kumnunua Declan Rice kwa Pauni 105 milioni.

Awali staa huyu alikuwa akihusishwa na Arsenal, lakini waliachana naye na kumsajili Rice. Kwa sasa Chelsea inamwangalia staa huyu kama mbadala wa N’Golo Kante.

Mwinyi Zahera aanza makeke Coastal Union
Usajili wa Young Africans bado CAF