Rapa wa kike anaefanya vizuri na wimbo wake ‘Sielewi’ aliomshirikisha Soprano, Chemical ametunisha misuli ya kipaji chake na kueleza kuwa yeye ndiye rapa bora zaidi wa kike Tanzania katika kipindi hiki.

Chemical aliiambia The Playlist ya 100.5 Times Fm inayoendeshwa na Lil Ommy kuwa hajiweki nafasi ya pili na haoni wa kumtaja kuwa rapa bora zaidi wa kike kwa wakati huu kwa kuwa nafasi hiyo anaishikilia yeye.

Rapa hiyo ambaye wengi wamekubali uwezo wake na kumuita ‘dope female rapper in Tz’, amewatia moyo rapa wengine wa kike waliokata tamaa kutokana na vikwazo mbalimbali. Amesema ujio wake kwenye muziki wakati huu utawapa sababu zaidi rappers wa kike nchini kufanya vizuri.

“Nimekuja kuwarudisha rappers wa kike, kwa wale ambao waliacha nimekuja kuwapa sababu za kuwarudisha,” alisema Chemical na kuongeza kuwa hata wale wasanii wa kike ambao bado hawajafika pale wanapotaka lakini wameanza kukata tama, yeye amekuja kuwapa sababu zaidi za kufanya vizuri kwenye game.

Katika hatua nyingine, rapa huyo mwenye muonekano wa ‘ki-tomboy’ alieza kuwa ingawa baadhi ya watu wanahisi kwa muenekano wake kama rapa wa kike atakuwa anatumia bangi, yeye hajawahi kutumia na hatarajii kuwa mfuasi wa mmea huo unaochanganya vichwa vya vijana wengi.

Aliwataka wIMG-20150706-WA0010asanii wa kike kuacha kupenda mteremko kwa kuwa hali hiyo inaweza kuwapelekea kuanguka kwenye mikono ya wanaume wanaowatumia kwa ahadi za kuwasaidia kimuziki.
“Wasichana wengi wanapenda slop, wasipende slop, wasichana tunatakiwa kuhusle kama wanaume,” alifunguka.

Sielewi ni single ya kwanza kubwa ya rapa huyo ambaye aliwahi kureko zaidi ya nyimbo kumi na tisa, ina video nzuri inayofanya vyema kwenye vituo mbalimbali vya runinga nchini.

Steven Gerrard Akaribishwa Kwa Pombe Marekani
Kikwete: Msimchague Huyu, Mnyanyapaeni