Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) kimesema kimefurahishwa na ahadi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambalo limeahidi kubeba majukumu ya kuiweka kambini timu ya taifa ya Netiboli (Taifa Queens).
Taifa Queensi inatarajiwa kuingia kambini wakati wowote, kujiandaa na mashindano ya Afrika ambayo yatafanyika kuanzia Agosti, mwaka huu jijini Kampala, Uganda.
Akizungumza Dar es Salaam Katibu Mkuu wa CHANETA, Rose Mkisi amesema hiyo itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo nchini kwa serikali kupitia BMT kubeba majukumu ya kuiweka kambini Taifa Queens.
“CHANETA tumeipokea taarifa hiyo ya BMT kwa furaha kubwa, kwani hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa BMT kufanya hivyo katika historia ya mchezo huo nchini,” amesema Katibu Rose.
Amesema I kinachoendelea sasa CHANETA inamsubiri Katibu Mkuu wa BMT, Neema Msitha ambaye yuko nje ya Tanzania ili atakaporejea wajadiliane kuhusiana na bajeti ambayo walishaíwasilisha.