Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi la polisi linamshikilia mhudumu wa Hoteli ya Sleep Inn na mkazi wa Mwananyamala kwa kopa, Erick Francis Chilemba (30) baada ya kukutwa na sare za polisi, silaha, cheo cha koplo na pingu.
Mambosasa amesema kuwa jeshi la polisi lilipokea taarifa hizo toka kwa msiri kuwa mtu mmoja anatumia sare za jeshi la polisi kuwakamata watu na kuwafunga pingu kuwatishia bastola ili kufanikisha kupora mali maeneo mbalimbali ya jiji.
”Baada ya kupata taarifa hizo jeshi la polisi lilianza ufuatiliaji mara moja na kuweka mtego mnamo tarehe 21, Mei 2018 majira ya saa nne usiku huko Mwenge Bamaga Polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo” amesema Mambosasa.
-
JPM atoa shavu jingine Bima (TIRA)
-
Heche adai TANESCO haitapata faida milele, mkataba wake na Songas ni wa kihuni
Mambosasa ameongezea kuwa baada ya kufanya nae mahojiano mtuhumiwa alikiri kumiliki sare na vifaa mablimbali vya jeshi la polisi na kukubali kuwapeleka askari hadi nyumba anayoishi.
Ambapo baada ya kufanya upekuzi kwenye nyumba anayoishi alikutwa na sare za jeshi la polisi, pingu, cheo cha koplo wa polisi, mfuko wa kuhifadhia bastola na bastola aina ya GLOCK 17 ambayo imefutwa namba zake za usajili ikiwa haina risasi.
Aidha mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.