Sheria mpya ya kulinda faragha ya mtu barani Ulaya imeanza kutekelezwa huku ikikusudia kulinda faragha ya raia na kurekebisha jinsi makampuni yanavyo kusanya, kutumia na kuhifadhi taarifa zao.
 
Sheria hiyo mpya imeanza kutumika wakati ambapo kampuni kubwa ya mitandao ya jamii Facebook ikiwa inakosolewa nchini Marekani kwa kashfa ya kushindwa kulinda faragha za watu.
 
Aidha, sheria ya Kulinda Taarifa Kwa Jumla ya Umoja wa Ulaya (GDPR), ambayo inakuwa iko juu ya sheria mbalimbali za nchi moja moja zilizokuwepo tangu mwaka 1995, inazitekeleza sheria hizo kwa nguvu zaidi.
 
Tofauti kubwa iliyopo kwasasa sheria hizo zinataka makampuni kueleza wazi jinsi wanavyokusanya na kutumia taarifa hizo. Matokeo yake, kampuni zinaondoa misamiati wakati wakizifanyia marekebisho sera zinazosimamia faragha za watu.
 
  • Kiumbe wa ajabu awavuruga Wanasayansi, washindwa kumtambua
 
  • Zaidi ya watu 100,000 huumwa na nyoka, WHO yapitisha azimio
 
  • Polisi wamvua nguo mwanamke wakidai wanafanya uhakiki
 
Hata hivyo, Sheria hizo mpya zinatumika katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya lakini pia zitaathiri biashara zote kubwa na ndogo nchini Marekani

Cheo cha koplo, Pingu vyamtia mbaroni mhudumu wa hoteli
Polisi wamvua nguo mwanamke wakidai wanafanya uhakiki