Jeshi la China limezindua siku tatu za mazoezi makubwa ya kijeshi huko Taiwan, ililenga kuizingira Taiwan kutokana na mvutano uliopo kisiwani humo baada ya mkutano wa Rais Taiwan Tsai Ing-Wen na Kevin McCarthy na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani nchini Marekani.
Msemaji wa Jeshi la China, Shi Yi Uzinduzi amesema uzinduzi huo umefanyika hii leo Aprili 8, 2023 ambapo Manowari nane za kivita na ndege 42 za kivita zimeonekana karibu na kisiwa hicho ambapo luteka hii ya siku tatu iliyoandaliwa na Beijing hutumika kama onyo kubwa dhidi ya ujumuishaji kati ya vikosi vya kujitenga vinavyotafuta uhuru wa Taiwan na vikosi vya nje.
Ndege za kivita za Jeshi la Watu wa Ukombozi wa China (APL), zikifanya mafunzo ya pamoja karibu na kisiwa cha Taiwan. Picha ya Gong Yulong / Xinhua.
Awali, Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen alisema, “Ndege 29 zimezidi mstari unatenganisha China na Taiwan na vitendo hivi visivyo vya kawaida katika miaka ya hivi karibuni, tumekuwa tukikabiliwa na upanuzi unaoendelea wa kiimla, tutaendelea kufanya kazi na Marekani na nchi zingine kutetea maadili ya uhuru na demokrasia.”
Mazoezi hayo yanakuja ikiwa ni siku chache baada ya ziara ya Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen nchini Marekani, ambapo alikutana Spika wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani, Kevin McCarthy Jumatano Aprili 5, 2023 na Beijing iliahidi kulipiza kisasi kutokana na kukosekana kwa uhusiano rasmi unaofanya Marekani kukipa kisiwa hicho msaada wa kijeshi.