Huduma baada ya kuzaa kwa mama inapaswa kukabiliana na mahitaji yake maalum, kuanzia saa moja baada ya kutoka kwa kondo na kuendelea kuwepo kwa wiki sita zinazofuata, huduma hii ni pamoja na kugundua mapema na kutibu matatizo, utoaji ushauri kuhusu unyonyeshaji, upangaji uzazi, chanjo, na lishe bora wakati wa ujauzito.

Ili kufanya huduma baada ya kuzaa kwa mama iwe ya kawaida, unashauriwa kutumia uchunguzi, ushauri na kadi za kurekodi huduma baada ya kuzaa ili huhakikisha kwamba umepitia hatua zote muhimu katika kumsaidia mama aliyejifungua.

Hapa chini nimeandaa mambo kadhaa ambayo wataalamu wa afya ya mzazi wanashauri, kwani imekuwa ni desturi mama anapojifungua ndugu, jirani rafiki kuwatembelea wazazi, inaweza kuwa kwa kujua au kutokujua kufanyika kwa mambo haya hasa pale tunapomtembelea mama aliyetoka kujifungua kama ifuatavyo.

Usipake marashi au mafuta makali, hii ni maalumu kwa mama mwenyewe na mtoto kwani harufu kali zinaweza kumchefua mama mjamzito na kumsababishia mtoto mafua makali

Tusaidie kazi pale inapobidi.

Tusikae muda mrefu.

Tuwatie moyo wazazi na sio kuwakatisha tamaa, kwani unapomtia moyo mzazi inamsaidia kutulia na kumfanya mzunguko wake wa damu ukae sawa na upatikanaji mzuri wa maziwa kwa mtoto, kwani wazazi wengi wanakumbwa na tatizo la maziwa kushindwa kutoka zipo sababu nyngi zinazoleta hali hii ikiwemo mawazo, uoga, hivyo tujitahidi kuwa chanya sana na kuwatie moyo wazazi ili waweze kulea vizuri na kuendelea kuona mtoto ni baraka nyumbani kwake.

Usitoe ushauri bila kuulizwa, wapo watu wenye tabia za kujifanya wanajua kila kitu hivyo hutaka pia kushauri kila kitu, sasa wataalamu wanashauri kama hujaulizwa jambo na mzazi basi usitoe ushauri kwa uelewa wako au mazoea yako, kwani kila mtu yupo tofauti na mwingine, kama jambo ni kubwa sana ni vyema ukamshauri mzazi afike hospitali kuonana na daktari.

Kama unaumwa subiri upone ndio ukamtembelee, hii ni muhimu sana, hili ni kuepusha kusababisha maambukizi ya magonjwa kwenfda kwa mama na mtoto kwani wakati huo mama na mtoto ni rahisi sana kudhulika na kupokea magonjwa kutoka kwa watu wengine.

Using’ang’anie kubeba mtoto, kumbuka kunawa mikono na usimbusu mtoto

Mwisho usimtake wala kumlazimisha mama mzazi afanye unachokijua wewe

 

NEMC yafunga machinjio ya msalato kwa muda usiojulikana
DC alia na wilaya yake kuburuza mkia uandikishaji wa CHF iliyoboreshwa