Jina la Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia na Klabu ya Simba SC Clatous Chotta Chama limejumuishwa katika orodha ya wachezaji iliyotumwa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’, kwa ajili ya ushiriki wa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2022/23.
Simba SC na Young Africans zitaiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa, huku Azam FC na Geita Gold FC zikishiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
Chama ambaye alisajiliwa Simba SC kwa mara ya pili wakati wa Dirisha Dogo la usajili msimu uliopita akitokea kwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika RS Berkane, hakucheza michuano ya Kimataifa akiwa na klabu hiyo ya Msimbazi, kutokana na jina lake kusajiliwa CAF kupitia klabu hiyo ya Morocco.
Kutumwa kwa jina la Kiungo huyo ni dhahir Chama atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC ambacho kitaanza Mchakato wa kusaka Ubingwa wa Afrika kwa kucheza na Mabingwa wa Malawi Nyassa Big Bullet, ambayo itakua nyumbani kati ya Septamba 9-11 na baadae mchezo wa mkondo wa pili utapigwa Uwanja wa Mkapa kati ya Septamba 16-18.
Mshindi wa mchezo huo atacheza na Mshindi wa mchezo katika ya Red Arrows ya Zambia dhidi ya Premero di Agosto ya Angola, na atakayeibuka Mshindi atatinga moja kwa moja katika Hatua ya Makundi.
Mbali na Chama majina mengine ya wachezaji wa Simba SC yaliyowasilishwa CAF kwa ajili ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ni Aishi Manula, Beno Kakolanya pamoja na Ally Salim.
Mabeki: Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Israel Mwenda, Gadiel Michael, Joash Onyango, Mohamed Ouattara, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Hennock Inonga pamoja na Nassoro Kapama.
Viungo: Victor Akpan, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute, Peter Banda, Pape Sakho, Jimmyson Mwanuke, Augustine Okrah, Clatous Chama pamoja na Nelson Okwa.
Washambuliaji: John Bocco, Kibu Dennis, Moses Phiri, Habib Kyombo pamoja na Dejan Gegeorgevic.