Meneja wa Habari na Mawasilino wa SImba SC Ahmed Ally amefichua kufikiwa kwa makubalino kati ya Uongozi wa Klabu hiyo na Kiungo kutoka Zambia Clatous Chota Chama.
Pande hizo mbili zilikuwa katika mazungumzo ya kusaini mkataba mpya, kufuatia mkataba wa awali wa kiungo huyo kutarajia kufikia kikomo mwezi Januari 2024.
Ahmed Ally amefichua siri hiyo kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii akieleza kuwa, Chama amekubali kusalia Simba SC, na atakaporejea nchini Tanzania atasaini mkataba mpya wa miaka miwili.
Chama alisaini mkataba na Simba SC mwezi Januari 2021 aliposajiliwa tena klabuni hapo akitokea RS Berkane ya Morocco, ambako alishindwa kucheza soka lake, kutokana na mazingira ambayo alidai hayakuwa rafiki kwake na familia yake.
Ahmed Ally ameandika: Chama amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuitumika Simba Sports Club
Mkataba utasainiwa akirejea Tanzania baada ya majukumu ya timu ya taifa na mapumziko kabla ya Pre Season.