Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amezungumzia lengo kuu la kuleta shindao kubwa la kutafuta vipaji Afrika Mashariki litalojulikana kama East Africa got Talent na kuhusisha vipaji vya aina zote.
Amesema kuwa mara zote kumekuwa na mashindano ambayo ni ya kuimba tu bila kuangalia kuwa kuna vipaji vingine tofauti na kuimba lakini ameongeza kuwa clouds ndio iliyokuja na ‘agency’ ya kwanza ya masuala ya mitindo hiyo miaka 22 iliyopita.
Ameongea kuwa Clouds iliwasiliana na serikali juu ya kufanya fainali hizi apa nyumbani lakini kulikuwa na sababu za msingi kuipeleka Kenya moja ikiwa ni miundombinu inayoruhusu uzalishaji wa tukio hilo ambapo fainali za EAGT zitafanyika nchini Kenya huku washiriki wakitoka katika nchi nne Tanzania, Kenya Uganda na Rwanda
Waziri wa habari sanaa na michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa East Africa Got Talent (EAGT) ni tukio muhimu sana katika kuitangaza nchi yetu na vivutio vyake.
Aidha amewapongeza Clouds media kwa mara nyingine tena wametutoa kimasomaso katika kuitangaza Tanzania na kuibua vipaji kwa vijana.
Record lebal ya kwanza ya muziki ilitokea ndani ya Clouds na baadae kituo cha kwanza cha burudani tulianzisha sisi kwahiyo tumeona huu ni wakati muafaka kwa sisi kuwa wakwanza kuleta shindano kubwa Zaidi duniani, amesema kusaga
Kampuni ya Rapidblue ndio wanazalishaji vipindi vya South Africa Got Talent na matukio mengine makubwa ambapo watashirikiana na Clouds media katika uzalisha wa matukio yote ya East Africa Got Talent