Uongozi wa Klabu ya Coastal Union umetoa taarifa ya kusikitishwa na Mjadala unaoendelea hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii, uliopachikwa jina la Fair Competition ambao unaihusu kampuni ya GSM.

Kampuni ya GSM inatajwa kwenye mjadala huo, kufuatia udhamini/ufadhili iliouweka kwenye klabu za Coastal Union, Young Africans na Namungo FC.

Taarifa iliyotolewana Uongozi wa Coastal Union na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii leo Jumanne (Novemba 09) imeeleza kuwa, Mjadala huo hauna afya na hauleti tija kwenye soka la Tanzania kwani utafanya kudumaza soka la Tanzania kutokana na Wadhamini kujiondoa.

Kutokana na hali hiyo Uongozi wa Coastal Union umewataka wachambuzi pamoja na watu waliopo kwenye vyombo vya habari kutumia nafasi walizonazo kuwashawishi wawekezaji kwenye soka la Tanzania na sio kuwavunja moyo.

Franco Pablo: Nimefurahi kupata kazi Tanzania
High School ya Harmonize ingefanikiwa kama angezingatia haya