Nahodha na kiungo wa zamani wa klabu ya Arsenal Francesc Fàbregas Soler ameonyesha moyo wa upendo katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, yanayoendelea duniani kote, kwa kukubali kusamehe mshahara wake wa miezi minne.

Kiungo huyo ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya AS Monaco ya Ufaransa, amechukua maamuzi hayo baada ya uongozi wa klabu hiyo kutangaza kuwakata asilimia 30 ya mshahara wachezaji wake, katika kipindi hiki.

Asimilia 30 ya wachezaji wengine wa AS Monaco na mshahara wa miezi minne wa Fabregas, itatumika kwenye vita ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ufaransa, pamoja na kulipa mishahara ya wafanyakazi wengine wa klabu hiyo.

Kwa juma Fabregas anapokea mshahara wa Pauni laki moja na thelathini (130,000), hivyo kwa hesabu ya mshahara wake wa miezi minne utakaopelekwa kwenye vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona na kulipa mishahara ya wafanyakazi ni Pauni milioni mbili na elfu themanini elfu (2,080,000).

Kama itakumbukwa vyema wakati Fabregas anaondoka Arsenal kwenda FC Barcelona kwa dau la Euro milioni 39, alikubali kulipa Euro milioni 5 ili kukamilisha ada yake ambayo haikutimia kutokana na mabingwa hao wa Hispania kulipa Euro milioni 34.

Fabregas alilipa kiasi hicho cha pesa kutoka kwenye makato ya mshahara wake, ili atimize jukumu la kucheza kwenye kikosi cha FC Barcelona ambacho kwa wakati huo kilikua bingwa wa Ulaya.

Fabregas alisiani mkataba wa miaka mitano alipojiunga na FC Barcelona, ambapo kila mwaka alipaswa kukatwa Euro milioni moja ili kulipa deni hilo.

Kwa mantiki hiyo inadhihirisha wazi Fabregas amekua na moyo wa kujitolewa, linapokuja suala la kukamilisha maisha yake ama maisha ya wengine.

Tanzia: Mbunge Ndasa afariki dunia, Ndugai ahairisha vikao vya Bunge
Maisha ya Ndemla ni bora kuliko matamanio yenu