Rais, Dkt. Joh Pombe Magufuli ametangaza kuwa endapo hali ya maambukizi ya virusi vya corona itaendelea kupungua kama ilivyo sasa, siku za hivi karibuni ataruhusu vyuo vifunguliwe na michezo iendelee.
Akitoa salamu zake baada ya kushiriki ibada ya jumapili mjini chato amesema idadi ya yagonjwa wa covid -19 katika vituo vya afya imepungua sana jambo ambalo Mungu amejibu maombi ya Watanzania.
” Na kwa hali inavyoendelea ikiwa hivi nimepanga kufungua vyuo, lakini nimepanga pia sisi kama taifa kuruhusu michezo iendelee” amebainisha Rais Magufuli.
Katika ahatua nyingine amesema shughuli za utalii ziataanza rasmi, tayari kuna ndege zimejaa nafasi na hakutakuwa na vizuizi vya karantini kwa watalii, wakipima joto la mwili na kuona hawana dalili wataruhusiwa kwenda kutalii.
Amesisitiza kuwa Uchumi utaendelea kupewa kipaombele na serikali yake haitaweka amri ya kutotoka nje kama inavyofanywa na mataifa mengine na kwamba Mwenyezi Mungu atasaidia katika kulikabilia janga la corona.
Amesema wale wanaowawekea raia wao masharti ya kutotoka nje waendelee kufanya hivyo, Tanzania itawasaidia na chakula watakapomaliza na kusisitiza kwamba serikali yake na Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na ile ya SADC zitaendelea kushirikiana.