Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba, Senzo Mazingiza amesema bado ni mapema kuanika hadharani orodha ya wachezaji wanaoachwa na klabu hiyo, kwa maslahi ya kuboresha kikosi kwa msimu ujao wa ligi.

Klabu ya Simba imekua ikihusishwa na mipango ya kuwasajili baadhi ya wachezaji wa ndani na nje ya nchi, hali ambayo inadhihirisha ni lazima kuna badhi ya wachezaji wataachwa mwishoni mwa msimu huu.

Mazingiza amesema kwa sasa hawawezi kuwataja wachezaji gani watawachwa, lakni itakapofika mwishoni mwa msimu huu lazima kuna wachezaji wataondoka na wapya wataingia.

Kiongozi huyo amedai kuwa klabu hiyo haitafanya usajili wa wachezaji wengi zaidi ya kuboresha sehemu chache ambazo wameziona zina shida.

“Kuna baadhi ya wachezaji wataachwa mwishoni mwa msimu huu, lakini kwa sasa ni mapema mno kusema lolote kuhusu mpango huo, msimu bado unaendelea na kila mmoja ana wajibu wa kuitumikia Simba ili kufikia lengo la kutwaa ubingwa.”  Alisema Mazingiza

Pamoja na kusema hivyo ripoti ya kocha Sven aliyoiwasilisha kwenye Bodi inataka kusajili wachezaji 6 wapya ikiwa wachezaji 3 wa nje na wachezaji 3 wa ndani.

Iwapo Simba itasajili wachezaji 3 wapya wa nje wachezaji wawili Kati ya Tairone Santos (Brazil), Gerson Fraga (Brazil) na Sharaf Shiboub (Sudan) lazima wataachwa.

Waziri ahimiza wamiliki wa viwanda kukata bima za moto
Corona Tanzania: Vyuo, Michezo kufunguliwa, Utalii bila karantini