Wanandoa, Boniphace Mwita (49) na mkewe, Rosemary Jenera (41) wakazi wa Tababta Kimanga, Jijini Dar es salaam wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kutoa lugha hatarishi kwa kupotosha jamii kuhusu ugonjwa wa Corona.

Wakisomewa mashtaka yanayowakabili mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Vicky Mwaikambo na wakili wa serikali mwandamizi, Mkunde Mshanga akisaidiana na Wankyo Simon wanadaiwa kutenda kosa hilo Machi 20 mwaka huu.

Imeelezwa kuwa washtakiwa hao wakiwa kwenye usafiri wa umma (daladala) aina ya Toyota Coaster lililokuwa linatokea Tabata kwenda Muhimbili huku kikiwa na abiria wengine.

Matamshi wanayodaiwa kuyatamka wanandoa hao ni ” Ugonjwa wa corona, serikali inadanganya hakuna ugonjwa wowote na imefunga shule kwakuwa haina hela na ada za kusomesha watoto bure”

Hata hivyo washtakiwa walikana kutenda kosa hilo na wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowataka kuwa na wadhamini wawili kila mmoja mwenye barua za utambulisho na watakaosaini bondi ya Tsh. milioni tano.

Wakenya kupewa fedha za ruzuku ya athari za corona
Corona Marekani: vifo vyaongezeka, maambukizi yapungua