Mshambuliaji wa Juventus FC Cristiano Ronaldo anafanyiwa uchunguzi kubaini kama alikiuka taratibu za afya wakati alipofanya safari kutoka Italia kwenda Ureno.
Waziri wa Michezo nchini Italia Vincenzo Spadafora ameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, anashukiwa alifanya makosa, huku majibu ya wali yakionesha na hakufuata taratibu.
“Wakati akiondoka Ronaldo hakuheshimu taratibu, na kuna uchunguzi unafanyia kuthibitisha hili” amesema Vincenzo Spadafora.
Ronaldo alikutwa na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid 19) alipokuwa nchini kwao Ureno, lakini siku chache baadae alirejea Italia kwa usafiri wa ndege binafsi.
Awali, Mkurugenzi wa michezo wa Juventus FC, alikanusha kuwa mshambuliaji huyo hakukiuka masharti yeyote na alisafirishwa kwa ndege maalumu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.
Uchunguzi unaofanyika ni kuangalia sakata zima tangu Juventus FC walipopata visa vya Corona, na namna Ronaldo alivyofanya safari zake, ikiwa atathibitika kuvunja taratibu zilizowekwa na mamlaka za Afya basi anaweza kuwajibishwa.