Mwenyekiti wa klabu ya Crystal Palace Steve Parish amethibitisha taarifa za klabu hiyo kuwa kwenye mkakati wa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa pembeni Wilfried Zaha, ili kuangalia uwezekano wa kumsainisha mkataba mpya.
Zaha, mwenye umri wa miaka 24, alisaini mkataba wa miaka mitano aliporejea klabuni hapo, akitokea Man Utd mapema mwaka 2015.
Mshambuliaji huyo ambaye aliamua kurejea nyumbani Ivory Coast akitokea England, alifunga moja ya mabao ya ushindi siku ya jumamosi wakati wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Chelsea waliokubali kichapo cha mabao mawili kwa moja.
Parish alithibitisha taarifa hizo, alipohojiwana shirika la utangazaji la Uingereza BBC, ambapo alisema uongozi wa Crystal Palace unaamini mpango huo utafanikiwa.
Wakala wa Zaha ameshaweka bayana mpango wa mchezaji wake kuwa mbioni kusajiliwa na klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo ipo tayari kutoa dau la Pauni milioni 15.
Zaha kwa mara ya kwanza aliitumikia Ivory Costa katika fainali za Afrika zilizofanyika mapema mwaka huu nchini Gabon.