Viongozi wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI) wametakiwa kuhakikisha viwanda vyote vinafuata mpango mahsusi wa kuzuia ajali katika sehemu za kazi ujulikanao kama ‘Vision Zero’ ulioanzishwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).
Wito huo umetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, wakati akizungumza na viongozi wa CTI walipotembelea ofisi za OSHA jijini Dar es salaam,
“Taasisi yetu imekuja na mpango mahsusi wa kuzuia ajali katika sehemu za kazi ujulikanao kama ‘Vision Zero’ ambao
endapo utatekelezwa ipasavyo katika viwanda na sehemu nyingine kazi basi matukio ya ajali yatabaki kuwa historia,” amesema Mwenda.
Mkurugenzi Mtendaji wa CTI, Leodgar Tenga amesmea badada ya kutembelea ofisi hizo wanatarajia upande wa OSHA wameelewa changamoto ambazo viwanda vinakumbana nazo na wenye viwanda wameelewa nini wanapaswa kufanya katika kuteleza sheria.
“Tunafahamu kwamba OSHA ipo kwa mujibu wa sheria na ina kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba kunakuwa na usalama wa wafanyakazi katika maeneo ya kazi na wenye viwanda ndio wahusika wakubwa sana katika hili na kwasababu hiyo tumekuja ili kuona ni kwa jinsi gani tutahakikisha wenye viwanda wanatimiza matakwa ya OSHA,”
amesema Tenga.