Mke wa Afisa wa polisi, Derek Chauvin, ambaye alionekana kumkandamiza kwa mguu mmarekani mweusi na kupelekea kifo chake, amefungua jarada la kuachana na polisi huyo.

Mwanamama Kellie Chauvin kupitia kwa Wakili wake ameeleza kufungua jarada akitaka kuachana na Afisa huyo wa Polisi.

Wakili wa Mke huyo amesema Kellie amesikitishwa sana na kifo cha Floyd na yupo pamoja na familia, wapendwa na kila mmoja anayeomboleza kifo hicho.

Ingawa Kellie hana watoto na Derek, ila ana watoto aliozaa awali kabla ya kuolewa na Derek na ameomba watoto hao, wazazi wake na ndugu zake wapewe faragha na ulinzi kwa muda huu.

IKumbukwe kuwa Kufuatia kuuawa kwa George Floyd na Polisi, Maafisa wa Polisi 4 waliohusika na tukio hilo wote walisimamishwa kazi huku Watu wakiandamana kupinga mauaji hayo.

Jana Afisa wa Polisi, Derek Chauvin ambaye alionekana kwenye video akiwa amemkandamiza Floyd shingoni kwa kutumia goti alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji daraja la 3 na mauaji ya bila kukusudia daraja la 2.

Habari picha: Rais Magufuli akikabidhi Tausi kwa marais wastaafu, Maria Nyerere
CTI watakiwa kutekeleza mpango wa OSHA ‘Vision Zero’