Klabu ya Universidad Nacional ‘Pumas’ ya nchini Mexico imethibitisha kuvunja Mkataba na Beki wa zamani wa FC Barcelona, Dani Alves kufuatia kuhusishwa na tuhuma za kumnyanyasa kijinsia Mwanamke mmoja katika klabu ya usiku nchini Hispania.

Oumas ilimsajili ALves mwaka 2022 akitokea FC BArcelona ambayo ilimsajilikwa mara ya pili msimu wa uliopita (2021/22), akitokea São Paulo (2019–2021).

Rais wa michezo wa Pumas, Leopoldo Silva Klabu ya Pumas amezungumza hadharani na kuthibitisha taarifa ya kuvunjwa kwa mkataba wa Beki huyo.

“Klabu inasisitiza dhamira yake ya kutovumilia vitendo vya mwanachama yeyote, yeyote yule, ambavyo vinaenda kinyume na ari ya klabu na maadili yake,”

“Hatuwezi kuruhusu tabia ya mtu mmoja kuharibu falsafa yetu ya kazi, ambayo imekuwa mfano katika historia.” amesema Leopoldo Silva

Mtuhumiwa aliwasilisha malalamiko mapema mwezi huu na kesi bado iko wazi kuhusu uhalifu wa unyanyasaji wa kijinsia.

Alves mwenye umri wa miaka 40 aliiambia ‘Antena 3 TV’ mapema mwezi huu kwamba alikuwa kwenye klabu hiyo na watu wengine lakini alikanusha kuhusika na kitendo hicho.

“Nilikuwa nikicheza dansi na kufurahiya bila kuvamia nafasi ya mtu yeyote,” alisema. “Sijui huyu bibi ni nani … Ningewezaje kumfanyia hivyo mwanamke? Hapana.” alisema Alves

Nyota huyo wa Brazil aliichezea Barcelona kuanzia 2008-2016 na akarejea kwa muda katika klabu hiyo ya LaLiga kwa msimu wa 2021-22. Ameichezea timu ya taifa ya Brazil tangu 2006, akicheza mechi 126 na kufunga mabao nane.

Hizi hapa sababu za Chama kuachwa Dar
Leandro Trossard achekelea safari ya Arsenal