Shirikisho la Soka Barani Ulaya ‘UEFA’ limeanza kufanya uchunguzi dhidi ya Klabu ya Juventus ya Italia kwa ukiukwaji ambao unaowezekana kuwa wa leseni za vilabu ‘Club Licencing’.

Waendesha mashtaka mjini Turin, ambako klabu ya Juventus ina maskani yake Makuu, wamekuwa wakichunguza hesabu za Klabu hiyo, hususana za miaka mitatu iliyopita.

Wamekuwa wakichunguza maadili yanayohusishwa na usajili wa wachezaji kama ilivyoelezwa na mishahara ilitolewa wakati wa janga la COVID-19.

Jumatano (Januari 18) Klabuya Juventus ilitoa taarifa iliyodai kuwa, madai ya ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma “hayaonekani kuthibitishwa wala kulinganishwa” na “wanasalia na imani kwamba klabu imekuwa ikifanya ipasavyo kila wakati”.

Mapema mwaka huu, Juventus ilikuwa miongoni mwa vilabu vinane vilivyotiliwa shaka na UEFA, baada ya kushindwa kutimiza matakwa na vigezo vya fedha za matumini kwa msimu uliopita.

Taarifa ya UEFA imeeleza kuwa suluhu ya awali inaweza kubatilishwa na inaweza kuchukua hatua za kisheria ambayo inaweza kuona inafaa na kuweka hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za kiutaratibu za chombo cha UEFA kinachofuatilia matumizi ya fedha kwenye vilabu ‘CFCB’.

Taarifa ya UEFA ilisema: ” CFCB leo imeanza kufanya uchunguzi rasmi kwenye Klabu ya Juventus FC, kufuatia tuhuma za ukiukwaji wa Leseni za Klabu ‘Club Licencing’ na kanuni za Haki ya Kifedha.

Tayari Klabu ya Juventus imepokonywa alama 15 iliyozivuna katika Michezo ya Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’ na Mahakama ya michezo Nchini humo, kufuatia uchunguzi kuhusu michakato ya uhamisho wa wachezaji wa klabu hiyo pamoja na madai ya utumiaji wa mapato yasiyo ya kweli.

Juventus imeshushwa kutoka nafasi ya tatu hadi ya 10 kwenye msimamo wa Serie A.

Hata hivyo rufaa ipo wazi kwa klabu hiyo, ambayo ina rekodi ya kutwaa Ubingwa wa Italia mara 36.

Leandro Trossard achekelea safari ya Arsenal
Aliyepora shamba avamiwa na nyuki