Mkoa wa Dar es salaam umeibuka kinara katika ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha miezi tisa, Julai 2019 hadi Machi 2020 kwa kukusanya mapato ya Tsh Bil 126.77.
Hayo yamebainishwa na waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo wakati akitoa taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri kwa kipindi cha miezi tisa.
Jafo amesema kwa upande wa mikoa Dar es salaam imeongoza huku mkoa wa Rukwa ukishika mkia kwa kukusanya mapato ya shilingi Bil 6.34.
Amesema kwa upande wa mapato ya halmashauri za majiji, Halmashauri ilyoongoza kwa asilimia kulingana na makadirio iliyojiwekea ni halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambayo imefikisha asilimia 78 ya malengo yake.
Huku Halmashauri iliyoshika mkia ni ya Jiji la Dodoma ambayo imekusanya mapato kwa asilimia 55 ya makisio yake.
Kwa upande wa manispaa, Halmashauri ya manispaa ya Iringa imekuwa ya kwanza kwa kukusanya asilimia 100 ya makisio yake huku halmashauri ya manispaa ya Lindi ikishika mkia kwa kukusanya asilimia 49 pekee ya makisio yake.
Halmashauri za miji, NJombe imeongoza kwa kukusanya asilimia 130 ya makisio yake huku Handeni ikishika mkia kwa kukusanya asilimia 43 ya makisio yake.
Halimashauri za wilaya, Masasi imekuwa ya kwanza kuwa kukusanya asilimia 126 ya makisio yake huku shinyaga ikiwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 30 ya mapato ya ndani ya makisio yake ya mwaka.