Mmiliki mwenza wa Klabu ya Inter Miami CF, David Beckham, alitaja ushindi wa Penati wa timu yake dhidi ya Nashville SC katika fainali ya Kombe la Ligi ni usiku wa kipekee sana na akawasifu wamiliki wenzake, Jorge na Jose Mas kama washirika kamili.
Miami ilianza kwa bao la Lionel Messi na Fafa Picault akasawazisha dakika ya 57 na kuufanya mchezo huo kwenda kwenye mikwaju ya Penati ambapo Inter Miami ilishinda 10-9, hivyo kutwaa taji lao la kwanza tangu ilipoanzishwa mwaka 2020.
“Usiku wa leo (juzi) ulikuwa usiku wa kipekee sana, nadhani, si kwa klabu yetu tu, lakini kwa mashabiki wetu, wachezaji, familia zetu na wafanyakazi wetu wote ambao wamehusika katika safari hii nasi,” alisema Beckham.
“Lakini haikuwa rahisi. Usiku wa leo (juzi) ulikuwa mchezo mgumu sana. Nashville walifanya pambano la ajabu. Ilikuwa karibu sana mwishoni na pongezi kwao kama klabu, kama washirika na kama wachezaji, kwa sababu ilikuwa ngumu sana. MchezO mgumu. Lakini ulikuwa ni usiku wetu tu usiku wa leo (juzi).”
Beckham alikumbuka ugumu wake katika mikwaju ya Penati, ikiwa ni pamoja na kukosa katika raundi ya mtoano dhidi ya Ureno kwenye euro 2004.
“Mimi si shabiki mkubwa wa Penati,” alitania. Kisha akaongeza,
“Si rahisi kamwe kutazama michezo hii ikiisha hivi. Na kwa timu ambazo haziishii kushinda, ni wakati mgumu. Lakini kila Penati ya Miami ilikuwa ya ajabu.”
Beckham angeweza kuthamini ushindi huo zaidi ya mtu mwingine yeyote. Alianza harakati zake za kuweka timu ya upanuzi ya MLS huko Miamni mmamo 2014, lakini akakunbana na vikwazo vingi katika kutafuta wawekezaji zaidi na pia njia ya mkataba wa uwanja.
Lakini bahati yake ilianza kubadilika mnamo 2017 alipokuja Jorge na Jose Mas kama wamiliki Wenza.