Manchester United imeingia katika mbio za kuwania saini ya Mlinda Lango wa Brentford, David Raya kwa mujibu wa ripoti.

Hiyo ni baada ya Tottenham kugoma kutoa Pauni 40 milioni inayotakiwa Bentford.

Mlinda Lango huyo huyo mwenye umri wa miaka 27, yupo tayari kuondoka Brentford baada ya taarifa iliripoti Rata alikuwa tayari kutua jijini London baada ya Tottenham kuonyesha nia ya kumsajili kwani atakuwa mbadala wa Hugo Lloris.

United, ambayo ilimuambia Mlinda Lango wao chaguo la kwanza David de Gea kwamba haina uhakika kama ataendelea kuwa chaguo la kwanza kwa msimu ujao.

Aidha, taarifa ilitolewa na kituo cha televisheni cha Sky Sports Man United bado inasikilizia ofa iliyotajwa na Brentford, kwa sababu wanahofia kama kipa huyo ana thamani ya Pauni 40 milioni.

Wawakilishi wa Mlinda Lango huyo wametishia watamruhusu aondoke huru mwakani mkataba wake ukimalizika, kama hawatakubali kumsajli katika dirisha hilila usajili la kiangazi.

Meneja wa Brentford, Thomas Frank hana mpango wa kumuuza Raya, ambaye aliwagharimu Pauni 3 milioni ilipomsajili Blackburn mwaka 2019.

Hata hivyo uwezekano wa kipa huyo kuondoka katika kikosi hicho umekuwa ukichochewa zaidi na kiwango bora alichoonyesha ambacho kimezishawishi timu mbalimbali barani Ulaya kumsaka kwa udi na uvumba, jambo linalosukuma lolote kutokea.

DP World kuendeleza ajira za Watumishi Bandarini
Wema usiooza wamnufaisha Bibi mtoa msaada