Mwaka 2019, Bibi mmoja nchini Zimbabwe alitembea kwa muda wa saa mbili akiwa na mzigo wake mkubwa kichwani kwa ajili ya kwenda kuchangia waathiriwa wa maafa ya mafuriko nchini humo.

Mama huyo, hakuwa na fedha ya usafiri wa daladala kufika katika eneo hilo pamoja na mzigo wake, hivyo akaamua kuubeba kichwani.

Tajiri mkubwa nchini Zimbabwe, Strive Masiyiwa aliposikia habari ya mama huyu aliamua kumjengea nyumba na kumuunganishia na umeme wa mfumo wa Solar, ili awe na uhakika wa kupata umeme saa 24.

Lakini pia bilionea huyo akaanza kumlipa mshahara wa dola za Marekani $1,000 ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania milioni mbili, laki tatu na sabini na nane elfu, kila mwezi kwa maisha yake yote, usiache kutenda wema kwa wengine.

David Raya aziingiza vitani Man Utd, Spurs
Arsenal yakomalia mpango wa William Saliba