Beki kutoka nchini Canada Alphonso Davies kwa mara ya kwanza amefunguka namna alivyokataliwa FC Barcelona, huku akiweka wazi sababu ya kufanyiwa hivyo.

Davies ameeleza kuwa, aliwahi kukataliwa FC Barcelona na Rais aliyepita Josep Maria Bartomeu, kisa anatokea nchini Canada, jambo ambalo lilimuumiza sana hadi leo.

Beki huyo ni moja kati ya wachezaji bora duniani kwa nafasi yake ambaye timu nyingi za Ulaya zimekuwa zikimtolea macho.

Ulimwengu wa soka umemtambua Davies kupitia kipaji chake akiwa ni mkimbizi mzaliwa wa Ghana kwa wazazi wa Liberia, lakini yeye amepewa uraia wa Canada akiiwakilisha vyema nchi hiyo kimataifa.

Beki huyo amesimulia kwamba: “FC Barcelona walikuwa wananihitaji kuna wakati, lakini aliyekuwa rais wao (Bartomeu) alikuwa hanitaki sababu kubwa natokea Canada, siwezi kudanganya, kile kitu kiliumiza hisia zangu kwa kiasi kikubwa.”

Viongozi wa Dini wamuombea dua ya kheri Rais Samia
Pep Guardiola aitumia salamu Real Madrid