Klabu ya Everton imeendelea kujizatiti katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi, kwa kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Ajax Amsterdam Davy Klaassen.

Everton wamesajili kiungo huyo kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 23.6. Klaassen mwenye umri wa miaka 24 amejiunga na Everton kwa mkataba wa miaka mitano utakaofikia kimoko Julai 30 mwaka 2022.

Klaassen anaondoka Amsterdam Arena huku akiacha kumbukumbu ya kufunga mabao 49 katika michezo 163 aliyocheza, tangu alipopandishwa katika kikosi cha kwanza mwaka 2011.

Msimu uliopita Klaassen aliiongoza Ajax Amsterdam kutinga fainali ya michuano ya Europa League kabla ya kuchapwa mabao mawili kwa sifuri na Man Utd katika mchezo wa fainali uliochezwa mjini Stockholm, Sweden.

Pia aliiongoza Ajax Amsterdam kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uholanzi maarufu kama Eredevisie.

Mwaka 2016 Klaassen aligonga vichwa habari baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Uholanzi. Tuzo ambayo hapo awali iliwahi kuchukuliwa na wakali kama Ruud Gullit, Marco van Basten, Dennis Bergkamp na meneja wa sasa wa Everton, Ronald Koeman.

Matunzo ya 'Kangaroo Mother Care' faraja kubwa kwa wazazi Muhimbili
Oscar Garcia Achukua Mikoba Ya Galtier - St Etienne