Watoto wengi wanaozaliwa kabla ya siku na kutunzwa katika kitengo cha matunzo ya ‘Kangaroo Mother Care’ katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wanatoka salama na wakiwa na afya njema.

Rose Mathew, muuguzi katika hospitali hiyo amethibitha hayo na kueleza kuwa asilimia 98 ya watoto wanaopata huduma hiyo wanaimarika na kupata afya njema kabisa.

Amesema kuwa matunzo ya Kangaroo Mother Care yamesaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya siku na kwamba kitengo hicho kimekuwa faraja kubwa kwa wazazi.

“Hospitali inapata faraja kwasababu matunzo ya Kangaroo Mother care yameonyesha mafanikio makubwa katika hospitali yetu ikiwa ni njia mbadala ya matunzo ya watoto  wanaozaliwa kabla ya siku’’ amesema Rose Mathew.

Rose Mathew amesema hayo wakati akizungumza na wazazi ambao wamefika Kiliniki na kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika kwenye kitengo cha watoto ambao wapo kwenye matunzo ya Kangaroo Mother Care hospitalini hapo.

Wakizungumzia faraja zao wazazi waliofika hospitalini hapo, wametoa wito kwa uongozi wa hospitali kuendelea kuboresha huduma hiyo kwasababu kituo hicho ni cha taifa na kinahudumia watoto wengi.

 

Madega amvalia njumu Malinzi, atinga TFF
Davy Klaassen Atua Rasmi Goodison Park