Hatimaye nafasi ya urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepata wapinzani wawili hadi sasa baada ya mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Yanga, Iman Madega kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Madega amechukua fomu hiyo leo asubuhi katika ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam, baada ya Jamal Malinzi kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake hiyo ambapo awali ilionekana kama atakuwa hana mpinzani.

Malinzi ambaye ni rais wa sasa wa shirikisho hilo amechukua fomu ya kutetea nafasi yake huku Madega akijitosa kumng’oa katika nafasi hiyo.

Uchaguzi Mkuu wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 12, 2017 mkoani Dodoma.

 

Serikali kukabiliana na jangwa na ukame, miti milioni 280 kupandwa kila mwaka
Matunzo ya 'Kangaroo Mother Care' faraja kubwa kwa wazazi Muhimbili